Hanaku njaro ya kuhepa hongo industry….
Photo Credit:Standard Media Tingua risto
Kumbe kuna wadhii wamfanya kuchukua hongo, kukuwa janta permanent. Huku ukihustle vimwenda ndio uweze kupata mkwanja ya kusurvive, kuna msee anakutime, akuharass hadi uingize njeve na kutoboka kakitu.
Ukiwa dere kwa baro za Kenya, inakuwa kawa kuhandwa na akorino, kwa sababu washatambua njaro ya kuwai cheddars za haraka, kwa kutumia cheo yao vibaya. Ata baada ya bigi wa makarao, Inspector General Kimaiyo, kudai hanaku raiya anafaa kutoa bribe, hiyo operation bado inaendelea.
Siku hizi wadhii wa mathree hawako solo kwa category ya wale madere wanahandwa kwa baro. Sana sana mandai zile zimebeat ndio huonewa sana juu mavedi wanatambua lazima itakuwa na kasoro nifla. Na kwa ule anakosewa makosa, anaweza andikiwa traffic offence haiku, hadi akubali kukohoa ganji ya kubribe ofisa, kujitoa kwa hiyo noma.
Sa utapata mandai kibao zenye haziko road worthy bado zikiroam jiji, coz bora mwenyewe anatoa kitu kidogo. Kumaanisha tutazidi kurusha contribution kwa hiyo police fund na kufanya wasee kuomoka tukiona tu.