Hamilton ana top FP2
Photo Credit:Laurence Edmondson Tingua risto
Lewis Hamilton ndiye alitokea kama msee fastest sana kwa prako ya seko ya Japanese Grand Prix.
Alafu Nico Rosenberg alikuwa wa seko na 0.240s akiwa anagurumisha sido juu pia Hamilton anatumia sido, wa thado alikuwa Valtteri Bottas . And then wa forth alikuwa Jenson Button, akiwa anagurumisha MacLaren, mbele ya Sebbastian Vettel mwenye anagurumisha Red Bull ikiwa gari ya seko kukuwa na mbio after sido. Kim Raikkonen akiwa wa sita alafu anafuatwa na team mate wake Fernando Alonso kama wanagonya Ferrari, wakifuatiwa na Kevin Magnussen akiwa 8th place and then 9th Danill Kvyat.
After hiyo prako ya seco, kunao madere watatu walimake kiblanda. Na venye hizi race ni moja ya zile zimengojewa sana kwa calendar. Kamui Kobayashi akiwa ndiye champee wa Japan alikuwa wa fao kugonga barrier after ku oversteer baada ya kuanza tu.
Alafu Daniel Riccardo pia na yeseye akaingia barrier na aksi moja noma sana kama ana ingia kwa final chicane. Unfortunately aliweza kushika kibre na kupunguza speed. Ata in 2009, incident kama hii ilimfanyikia Tim Glock na ikamwai injury ya mgongo. Sasa ilibidi hiyo dinga kutolewa ndani ya track na ku cause red flag.
Esteben Gitierez pia na yeseye alikuwa involved kwa aksi inegi, baada ya kucrash kwa barrier. Ata hivyo flag ya seko ika inuliwa dakika kadhaa baada ya Jean-Erick kusmash dinga yake; Toro Rosso, ikiwa mara ya seko ana simama kwa race. And then Max Verstappen engine ya dinga yake ilirudi kuleta tafash.