Kumbe bado slavery inavuma!
Photo Credit:Google Tingua risto
Kumekuwanga na kashida dunia nzima, ya wasee kukosa kutoshana ikikam risto za mula. Lakini inakaa mambuus ndio husuffer zaidi kwa hii struggle ya kusaka mkwanja ya kulea famo. Alafu ni aibu vimost kwanza kwa hii enzi ya kujidai kukuwa Feminist.
Sa kuna reporter mjamo aligundua kuna madem huko Mauritius wenye wamechorwa janta ya kumekisha tisho za kupromote Feminism. Na saa hizo wanalipwa dollare jamo kwa kila idhaa wako waks. Mwanja ya siku jamo ata wakishikanisha haiwezi tosha kuboti tisho janamo yenye hukindwa $70.
Kuzidisha wanaishi kwa madorm kama keja, wakiwa mambuus kinde na six wanashare by force. Alafu wao hukuwa waks masaa kibao hadi hawawezi rudi mtaani kucheki famo zao. Na eti wanamekisha tisho zenye ziko na message inadai kuwatetea.
Inadaishwa hii risto bado iko under investigation, lakini tunajua poa wanataka tu ikuwe chini ya maji hadi isahalike, huku bado wakiendelea kukandamiza mamanzi wenye wanadai haki yao.