Machampee kutoka 254!
Photo Credit:Google Tingua risto
World Athletics Championships zikiwa zinaendelea husuko Beijing, tunacheki raiya wenye wanawakilisha 254 wameenda huko na ubaya. Wamekuwa wakiokota hizo Gold Medal ni kama mapaper. Enyewe kushow dunia wanamaanisha bizna sio magames.
Sector ya athletics bila kuringa, Kenya ndio ilikuwa inatop both kwa majamaa na madem. List ikiwa na Gold medal sita na zinengi tano kwa compe. Tunacheki majina kama; David Rudisha (800m), Nicholas Bett (400m), Ezekiel Kemboi (3,000m Steeplechase) na Vivian Jepkemoi Cheruiyot (10,000m).
Lakini ule ametujszz vimost, ni Julius Yego. Mwenye alichop techniques za javelin akitumia videsa za Youtube na this round ameweza kumark histo kwa kuwai Gold Medal pia. Akiwa na urefu ya 5ft9ins,na miaka mbaula na six, kutoka Nandi South County, enyewe amemekisha record mwenda sana.
Mvua ya 2010 ndio mara ya fao alitry kuduu javelin, lakini akafanikiwa na Bronze medal. Alizidi kutrain na akawa anamekisha record nira kila time. Raiya wa 254 wanamcheki kama hero na dunia nzima inabonga kumhusu vimajor. Riba ya vile kila yutman anaweza make it kupitia determination na kutaka kuchop vitu nira, inachangamsha kuruka.