Beef ya mapero kuangukia mtoi

January 21 2015 2:29pm     0 1884

Photo Credit:Google   Tingua risto

Alex Nash, mniaju wa miaka kobole kutoka  Plymouth, England, alijipata akidaishwa mkwanja na masa wa beshte yake juu ya kuhata birthday bash alikuwa ameitiwa.

Mapero wa Alex walipata mshangao, baada ya mtoi kurudi kutoka chuo akiwa na invoice ya thao mbwegz soh jamo na sixty bob. Bazenga wa Aleki alidhani ni jokes na kuenda kwa huyo matha kumshow hawawezi lipia kitu ya ufala hivyo.

Lakini inakaa huyo masa alikuwa na issues juu aliharass masake Aleki kwa Facebook akidai lazima walipe coz hawakucancel invitation. Hadi amekatsia ubeshte kati ya mtoi wake na Aleki, juu hawachezi pamoja tena. Na hii noma yote ni juu Alex aliopt kuenda kucheki magrandi wa kwake badala ya kuenda kwa bash ya beshte yake.

Imebidi hii risto kufikishwa kotiko juu wamelemewa kufikisha agreement. Ingekuwe wesewe, ungelipa ama ungezua kuruka?

Related Stories