Netherlands ika kung’uta Spain 5 - 1

June 18 2014 1:51pm     0 309

Photo Credit:Google   Tingua risto

Sasa kuna vile hii riba imetuget, vile Spain wakiwa hao ndio ma defending champions, na vile waliweza kukung’utwa dude kobole kwa jamo na team ya Netherlands kwa game yao ya fao. Mraiya most walibaki wamejam juu ya hio risto tu sana.


Spain walitingua madude na pena kupitia Xabi Alonso, baada Diego Costa kutegwa ndani ya box. Baadae Robin Van Persie aka equalize kupitia hedi moja noma sana, alafu kabla first half ikatike Arjen Robben akaweka Netherlands mbele na dude nyingine.


Second half Stefan de Vriji, akaweza tia ndani ya thado kutoka kwa free-kick ya Wesley Sneijder, bila kutupa idhaa Van Persie aka adisia dude yake ya seko na ku make scores kuwa 4-1. Baadaye, Robben aka tia ndani dude yake ya pili pia na ku make scores kuwa 5-1 naku seal hiyo win.


Mara ya last Spain kuwai tingwa ma dude kama hizi ilkuwa 1963 wakicheza na Brazil. Nakumbuka World Cup ya 2010, huko South Africa, ni hizi team mbili zilipatana kwa Finals, na Spain iliweza kushinda Netherlands na dude jamo na ku emerge kuwa winners 2010 World Cup.


Sasa saa hii, Netherlands ndio ile team wasee wanabonga sana kuihusu kulingana na ile game walicheza. Inasemekana Netherlands ni among ile team inaweza penya na hii trophy kama watazidi ku maintain game yao.


Hii game tunacheki ma defender wa Spain walikuwa na hard time kuweza hundle strike za Robben na Van Persie. Striker wa Spain Diego Costa alikuwa na hard time na mafans waki mrushia mkono, juu ali choose kuwa citizen wa Spain rather than Brazil. Kwa La Liga alikuwa the Best Player of the season, but kwa hii game haku perform venye alikuwa expected ku perfom.


Robin Van Persie ametinga dude kinde(10) kwa 9 international appearances, alafu naye Robben ametinga dude saba kwa seven international appearances. Still tukiwa kwa group stages tunacheki game next Netherlands itapatana na Australia, na Spain itapatana na Chile. Netherlands ina lead kwa Group B na points tatu, ikifwatwa na Chile, Australia alafu Spain ikiwa ya last bila point yeyote.

Related Stories