Wera ya loan siku hizi!

June 25 2014 1:32pm     0 1910

Photo Credit:Capital Fm   Tingua risto

Stude nifla anatambulika kama Katerina Christodoulou, aliamua kukwachu loan ya colle, na badala ya kulipia chuo, akaenda kuduu plastic surgery na hiyo mkwanja. Husuyu graduate wa English Literature, aliona heri kujinice na zaidi ya mita jamo ya loan ndio aweze kuget mwili ya super model. Na enyewe ukikemba mbisha zake, alitoboa kuget kile anadai inamfurahisha.

Lakini kile huyu mbuus hajajua ni venye anamezeshea wasee wale wanahitaji hiyo ganji kuweza kufilka yuni na kuchop. Juu inasemekana njaro za the British Higher Education, ni kuwai mastude loan kutoka kwa gava alafu wanafaa kulipa hiyo deni kwa miaka mbao na kobole, saa zenye wataangukia janta inawalipa zaidi ya $28,000 per year. Ambapo wakishindwa then hiyo deni itaendea taxpayers.

Sa juu tu wasee kama Katerina, wanapenda kupitia mashoti kwa life, inabaki raiya ndio wanaumia wakilipiana madeni. Ingekuwa hasapa 254, alafu HELB waskie hisihi fununu, si ingekuwa blanda bana! 

Related Stories