Trip ya K-shaka hadi Sweden

October 9 2014 10:58am     1 964

Photo Credit:Google   Tingua risto

Ni hard sana kusahau crew jamo ilijulikana kama Kalamashaka, ukibonga kuhusu Hip Hop ya hasapa 254. Hii rende ilikua made of Kama, Vigeti na Rawbar. K-Shaka ilikua jamo ya crew za fao kumekisha dunia nzima kudai kuskiza ngoma na kunotice talent zetu.

Ikifika 2002, walikuwa wamepenya na ngoma yao ‘Ni wakati’ ikarudi kukuwa anthem na ata ikawafanya kuwai deal ya kuenda tour na husuko Swido.  Wakiwa hiyo Swido walipatana na producer alijulikana kama Ken Ring, na akaproduce album nira.

CD yenyewe haikuwai skika, except track jamo tu ‘Fanya Mambo,’ yenye ilivuma sana hasapa 254 na ata ikawa recognized na Channel O ya SA. Videsa yake ilikua imbo lakini juu ngoma ilikuwa fyam,iliweza kuvuma kinyama.

Sa kuna documentary imechimbuliwa kutoka kwa archives yenye inaonyesha hiyo journey ya K-Shaka ninda ya Sweden. Umeikenga ama bado? Tushow ka unawatambua

Related Stories