Embassava kuchujwa waks

June 26 2015 7:21am     0 925

Photo Credit:Embassava   Tingua risto

Raiya most ya Eastlando inatambua hizi bu, sana sana ka ni raiya inapoa Jogoo Road, Doni, Tassia, Paipu ama Emba...bu za Embassava. Wale wasee wamepoa hizi area wamezitambua for a while juu zilianza na wanisa day za tene na ilikua a welcome move from mboko zilikua zinakorofisha raiya na mafare high. Kiasi yake bu zikaingia na wasee wakanice mabaya juu sasa queue zilianza kupungua pale tao.

Lakini kama kawa, kila kitu poa hua haikosi raiya moja mbili watakam kuharibu hio riba na after a while, kulianza kua na cases kadhaa za staff kukorofishana na wadhii, overcharging, rudeness ya staff na pia blanda ingine yenye iliwamulika mbaya. Hii ni vile msupa nifla alivuliwa nguo hasapo kwa rotejo ya Embassava, along Tom Mboya Street. Sasa after hio blanda, wamejipata tena kwa rada ya wadhii na in a negative light.

Jioni ya Thursday June 18th 2015, kuna bu yao jamo ilikua involved in an accident on Jogoo road na ilikua noma sana design wasee wawili waliuma pamba, na wengine wengi wakaumia. Hii ilikua after dere wa bu kupatana head on na bu ingine ya Forward Travellers Sacco. Hii aksi ilifanya NTSA kuingilia na kuchunguza hisizi sacco mbe. According to letter walichomoa kwa wasee wa media, NTSA wanadaisha ati kumepatikana blanda kadhaa na hii sacco zenye management imekataa kushughulika nazo na mpaka wazikalie chini ndio watapewa license ya operation.

Hii ni kumaanisha, from jana, Thursday 25th hawafai kua kwa ubaro. Hii yenyewe ni blanda kwa wadhii wa zile area zinategemea hii bu, sana sana Emba, Paipu na Doni juu hanaku bu mob zingine ziko kwa hio route. Lakini much as wasee watakua inconvenienced, hii ni riba poa juu safety ya umati ndio inafaa kua first na ni about time NTSA ifanye mambo kuskiza kilio cha haki juu wasee wamekua wakiumizwa sana kwa hizi ubaro na wasee wa mathree.

Mathree za mtaa yako ziko na blanda ka hii? Tuchapie unawakilisha route gani...

 

Related Stories