Masaibu za kustay ocha

November 5 2014 3:24pm     0 437

Photo Credit:Google   Tingua risto

Imekuwa ngori kwa mambuus wale wanastay mayadi za ocha, sana sana walifika age ya kunyesha. Hii ni coz wanapatanga shida za kuwai sanitary towels mbio. Inaweza kuwa juu hawawezi kuafford ama hanaku easy access.

Lakini kuna venye wameonekaniwa na hiyo ngori inaweza kuwatoka kiasi. Margaret Gachagua, akiwa wifey wa Governor wa Nyeri County, aliamua kuchukua hatua na kutembelea machuo za hiyo area. Alafu akalaunch a menstrual hygiene programme. Ambapo ita make sure kuna sanitary towels na ngotha zinafikia madem wako chuo ninda ya county.

Alidai kuna venye hii initiative ilikua imeanzishwa lakini wasee husahau kwamba haitoshi kupeana pads pekee. Lazima kuinclude mangotha hasapo juu ni hard kukuwa safi kama manzi akona ngotha jamo wakati ananyesha.

 Kuna efforts za kuinvolve county gava kuset budget ya kuangalia maslahi ya mambuus kwa hii riba. Lakini kwa wale wanajiskia kati ya raiya, bado wanaweza patiana donations za kuboti pads na ngotha za kupelekea hao mambuus wako ocha. Mpango sahii ni kuwa machuo soh tatu, salasa na three.  

Related Stories