Lazima masafara kusurvive…

May 6 2015 12:46pm     0 260

Photo Credit:Google   Tingua risto

Inakuanga feeling mbaya sana ikisemekana hutakiani place yoyote. Mara mob utapata wasee wakiamua kufanya vitu za ajaabu ndio wakuwe accepted na wadhii wengine. Lakini hisihi group ya refugees wamebeat odds za kila aina.

Inasemekana the Bajau, wakiwa raiya wamekuwa forbidden kukanyaga grao ya Malaysia, waliamua kujenga home juu ya ama ninda ya ocean. Keja zao zimemekishwa na mbao na makuti na wao husurvive wakidaka fish, octopus na lobsters.

 

Matime hawako kwa hizo keja zao, utawaget ninda ya handmade boats. Wamekaa ninda ya waba sana, njaro waniaju wao hawatambui aina tofauti ya maisha. Ata hawajawai enda chuo na wakajaribu kufika kwa grao wataget ‘land sickness’. Yaani kuskia kumwaora ama kufaint  juu uko kwa area hujazoea.

Wanawezanga kupiga biz na wasee waishi kwa grao lakini mara mob hizo exchange za essentials kama rice, waba na cladi bila kushuka kutoka kwa boat zao. Macho za waniaju zishazoea kuswim kwa woiyes ya salt na hadi wanaweza enda dufo ata 20 metres down bila kurudi juu kuwai hewa, wakiwa wanasaka seafood.

Maisha kwa raiya wa Bajau ni simple sana na ata kama hawana state ama country, wanazidi kusurvive. 

Related Stories